Walinda amani Umoja wa Mataifa wanaohudumu kwenye Ujumbe wa Umoja huo wa kulinda amani nchini DRC, wanaendelea kuisaidia nchi hiyo inapokabiliana na ukosefu wa usalama, vita, na janga la kibinadamu.
MONUSCO ilianzishwa mwaka 2010, ikichukua majukumu ya misheni za awali za Umoja wa Mataifa zilizoanza majukumu yake kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu miaka ya 1960.
Majukumu yake ni pamoja na ulinzi wa raia, kuwezesha wahudumu wa kibinadamu kutekeleza kazi zao, na kusaidia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika juhudi zake za kuimarisha utulivu na kuimarisha amani.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaunga mkono juhudi za kibinadamu kwa kuimarisha usalama na kuhakikisha ulinzi wa raia, hasa katika kambi za watu waliokimbia makazi yao.
Wanajeshi wa jeshi la serikali ya DRC, wakiwa kwenye mafunzo sambambana walinda amani wa Umoja wa Mataifa, ili waweze kukabiliana vema na changamoto za u salama mashariki wa nchi hiyo.
MONUSCO imesaidia pia kukarabati miundombinu ya barabara ili kuwezesha wananchi kutembea kwa uhuru na kusongesha biashara, moja ya eneo muhimu la maendeleo.