China ambayo mwezi huu wa Februari inashikilia kiti cha urais wa Baraza hilo, iliitisha mjadala huo wakati ambapo baadaye mwaka huu, Umoja wa Mataifa utatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amepata fursa ya kuhutubia mjadala huo akisisitiza kuwa mshikamano na majawabu ya kimataifa yanahitajika sasa kuliko wakati wowote ule” wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kuvuruga dunia, huku ukosefu wa usawa na umaskini vikiongezeka.
Amani bado inazidi kuyoyoma
“Kwa jinsi ambavyo Baraza hili linafahamu fika, amani inazidi kusogezwa mbali zaidi kiasi kwamba iko mbali kuifikia – kuanzia eneo linalokaliwa la wapalestina, oPt,hadi Ukraine, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kwingine,” amesema Guterres.
“Ugaidi na misimamo mikali inasalia kuwa vitendo vya kikatili vinavyoendelea kuweko. Tunaona kiza kinene cha ukwepaji sheria nacho kikitawala. Uwekezano wa vita vya nyyuklia bado uko – inasikitisha – na ni kitisho dhahiri kilichopo cha hatari.”
Teknolojia zinazoibuka kama vile Akili Mnemba au AI, nazo pia pia ni changamoto—k ama ilivyo ahadi yake isiyo na ukomo, inayoeweza kudidimiza na hata kuchukua nafasi ya fikra ya binadam, utambulisho wa binadamu na kumdhibiti binadamu.”Mkataba wa Zama Zijazo
Bwana Guterres amesema “changamoto zote hizi zinalilia jawabu ambalo ni majawabu ya kimataifa,” na kusema miongoni mwa majawabu hay oni
Mkataba wa Zama Zijazo , uliopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka jana.
Mkataba huo, “unalenga kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa dunia kwa karne hii ya 21na kujengeana upya imani,” katika ushirikiano wa kimataifa, Umoja wa Mataifa na
Baraza la Usalama.
Miongoni mwa vipengele vyake ni kusongesha uratibu ndani ya mashirika ya kikanda, na kuhakikisha ushiriki kamilifu wa wanawake, vijan na makundi ya pembezoni kwenye michakato ya kisiasa.
Mkataba huo unaweka bayana mpango wa uchechemuzi kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, na kuchechemua upya ahadi ya marekebisho ya mifumo ya fedha duniani iliyoundwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya dunia, ili iweze kuhudumia ipasavyo ulimwengu wa sasa.
Halikadhalika unajumuisha Mkataba wa Kimataifa wa Kidijitali unaotaka kuundwa kwa chombo cha kusimamia Akili Mnemba, AI, inayoruhusu nchi zinazoendelea kushiriki kwenye upitishaji wa maamuzi.
Marekebisho ya Baraza la Usalama
Mkataba huo wa Zama Zijazo pia unatambua kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima liakisi ulimwengu wa sasa na sio ulimwengu wa miaka 80 iliyopita, na unaweka kanuni za kuongoza marekebisho hayo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu.
Baraza lazima liongezwe idadi ya wajumbe na liwakilishe uhalisia wa sasa wa kijiografia, ilihali nchi ziendeleaa kuboresha mfumo wake wa utendaji ili liwe jumuishi, wazi, fanisi, kidemokrasia na wajibishi.
Guterres amerejelea kuwa masuala hayo yamekuwa yakizingatiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
Kutumia fursa ya sasa
“Huu ni wakati wa kutumia fursa iletwayo na Mkataba wa Zama Zijazo , na kufanya kazi pamoja ili kufikia maridhiano miongoni mwa makundi ya kikanda na nchi wanachama – zikiwemo zile zenye ujumbe wa kudumu kwenye Baraza – ili kusongesha mazungumzo baina ya serikali,” amesema Katibu Mkuu.
“Kila mara, natoa wito kwa wajumbe wa Baraza hili kumaliza mgawanyiko ambao unazuia hatua fanisi kwa ajili ya amani,” amesema.
Ameweka bayana kuwa wajumbe w aBaraza wameonesha kuwa kukubaliana kunawezekana, mathalani hoja za kupeleka misheni za operesheni za ulinzi wa amani na kuwa na majawabu ya pamoja kuhusu misaada ya kibinadamu.
Azma ya kulegeza misimamo
“Hata katika siku za kiza kinene Vita Kuu ya Pili ya dunia, kupitia uamuzi kwa pamoja na mashauriano ya kina ndani ya Baraza hili, yaliendelea kufanyika, licha ya kasoro zilizokuweko, mfumo wa usalama wa pamoja ulikuweko.”
Hivyo amesema, “nawasihi kurejesha tena msimamo kama huo, kuendelea kufanya kazi na kumaliza tofauti na kujikita katika kufikia maridhiano yanayotakiwa ili amani inayotakiwa ipatikane kwa kila mtu.”
Katibu Mkuu amesema ushirikiano ni suala muhimu sana kwenye Umoja wa Mataifa, na ukiongozwa na majawabu ambayo ni Mkataba wa Zama Zijazo, unaweza kuwa mbinu thabiti zaidi ya amani.
“Tunapoangalia changamoto zinazotuzunguka, nasihi nchi wanachama ziendelee kuimarisha na kuboresha mfumo wetu wa kimataifa wa kusaka majawabu,” amesema, na kuongeza kuwa “hebu na tuyafanye yakidhi malengo, yakidhi matakwa ya watu na yakidhi amani.”