Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

udadavuzi

Mzozo nchini Syria umesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao. (Maktaba)
© WFP

Kusaka amani Syria: Fursa kubwa, hatari kubwa

Kufuatia kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria, Jumapili ya tarehe 8 mwezi Desemba 2024, Syria imeingia katika kipindi cha sinfofahamu, na Umoja wa Mataifa utakuwa na dhima muhimu ya kuhakikisha mpito tulivu utakaosongesha hatua za kurekebisha taasisi, kuzifanya ziwe tulivu. Halikadhalika kuendeleza juhudi za kuleta pamoja makundi na pande mbalimbali ambayo yaliibuka baada ya kuanza kwa vita mwaka 2011.

Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, The Hague, Uholanzi
International Criminal Court

Udadavuzi: ICC imetoa hati za kukamatwa viongozi wa Israeli na Hamas: Nini kinafuatia?

Uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,  (ICC) kutoa  hati za kukamatwa  ikitaja madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant na Kamanda wa Hamas Mohammed Deif, kumeibua watu wengi kutaka kufahamu kuhusu mahakama hiyo, na nini kitafuatia. Hiki ndio tunachofahamu hadi sasa