Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© IOM/Robert Kovacs

Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao

Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi?

Sauti
5'3"
UN News

Tanzania yataja mambo ya kuzingatiwa ili ulinzi wa amani uwe na tija

Historia ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ulianza miaka mitatu tu baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa wenyewe. Na kutokana na umuhimu wa ulinzi wa amani kote duniani, shughuli hiyo imedumu kwa miaka yote hiyo 77 hadi sasa na bado ni muhimu lakini inaendelea kukumbwa na changamoto kama anavyofafanua Brigedia George Mwita Itang’are wa Tanzania, moja ya nchi 10 duniani zinazochangia zaidi vikosi vya ulinzi wa amani.

Sauti
3'51"
UN News

Redio imetusaidia kufikisha elimu kwa umma kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
3'12"
World Bank/Hendri Lombard

Juhudi za mahakama Tanzania kutekeleza Lengo namba 16 ya SDG

Leo katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania aanaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linatilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.

Sauti
3'57"
UNHCR Video

Tumetembea wiki mbili kufika kambini Bushagara lakini bado hapa si nyumbani - Mwamini

Kutana na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi. Kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu imekuwa mtihani mkubwa kwa wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi. Kupitia video ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Flora Nducha anafafanua zaidi katika Makala hii.

Sauti
3'33"
UNFPA Video

UNFPA - Wakimbizi zaidi ya 18,000 wa Sudan sasa wanaishi katika kambi ya Korsi CAR

Vita inayoendelea Sudan kwa zaidi ya miezi 18 sasa inaongeza wimbi la wakimbizi ndani na nje ya nchi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA. Shirika hilo linasema takriban wakimbizi 18,000 waliokimbia vita Sudan hivi sasa wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Korsi katika eneo la Birao, jimbo la Vakaga Katikati Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambako UNFFPA inawapatia huduma muhimu zikiwemo za aya ya uzazi. Flora Nducha anatujuza zaidi katika makala hii

Sauti
17"
World Bank/LayeproPhotos

Umeme wa uhakika wanufaisha wanafunzi na jamii nchini Senegal

Senegal, taifa lenye watu zaidi ya milioni 18.5 liko kwenye mwelekeo wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme. Benki ya Dunia inasema kiwango cha kupata umeme kwenye taifa hilo sasa ni asilimia 84. Wakati huu ambapo asilimia zaidi ya 30 ya jamii za vijijini hazina huduma hiyo, serikali kwa kushirikiana na wadau kama vile Benki ya Dunia na sekta binafsi imechukua hatua na mabadiliko yameanza kuonekana. Je ni yapi? Assumpta Massoi anaelezea kwenye makala hii.

Sauti
3'17"
UNEP

UNEP: Mradi wa UNREDD umekuwa mkombozi kwa mazingira na kwa wakulima DRC

Karibu nusu ya idadi ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wanategemea misitu kwa chakula, nishati, afya, riziki na huduma za mfumo wa ikolojia kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ambao ni takriban watu zaidi ya milioni 40. Kwa kulitambua hilo mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuai huku ukipambana na umasikini UNREDD unaleta nuru kwa raia hususani mashariki mwa nchi hiyo. Ungana na Flora Nducha kwa ufafanuzi zaidi katika makala hii.

Sauti
3'41"