Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Afrika

Wanawake mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini wakibeba chakula kilichowasilishwa na  Umoja wa Mataifa na wadau wake.
WFP

WFP yatahadharisha kuhusu tishio la njaa Mashariki mwa DRC  huku watu zaidi wakizikimbia kambi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani WFP, limerejelea kwa kiasi usambazaji wa misaada ya chakula katika sehemu za Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), likitoa msaada muhimu wa lishe kwa wastani wa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miezi 59 waliokumbwa na utapiamlo, huku mapigano ya wiki tatu yakizidi kuathiri vibaya upatikanaji wa chakula kwa wale walio hatarini.

Patrice Vahard, Mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Pamoja ya Haki za Binadamu, UNJHRO, nchini DRC, akiwa ziarani Beni, Kivu Kaskazini.
BCNUDH RDC

DRC: Majaji, mawakili mafichoni baada ya wafungwa kutoroka jela Goma, raia nao mashakani

Wakati waasi wa M23 ikiendelea kusonga mbele kuelekea ‘maeneo mengine ya kimkakati’ mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, baada ya kuteka miji ya Goma jimboni Kivu Kaskazini na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini Umoja Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu athari mbaya za kutoroka kwa wafungwa kulikoshuhudiwa Goma, pamoja na magereza makuu ya Kabare na Bukavu.

Mtoto akibeba maji kupitia eneo la kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kanyaruchinya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© UNICEF/Arlette Bashizi

Watoto wa DRC wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki, yaonya Kamati ya UN ya Haki za Mtoto

Watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanakabiliwa na janga lisilo na kifani, wakivumilia ukiukwaji mkubwa wa haki zao, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela, ukatili wa kingono, uandikishaji wa kulazimishwa na utekaji nyara unaofanywa na pande zinazohusika katika mzozo, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto imeonya leo jijini Geneva, Uswisi.