Mzunguko mpya wa chanjo ya Polio waanza Gaza
Mzunguko wa sasa wa kampeni kubwa ya chanjo ya polio huko Gaza, inayolenga karibu watoto wachanga 600,000, imeanza Jumamosi hii ya tarehe 22 Februari 2025.
Mzunguko wa sasa wa kampeni kubwa ya chanjo ya polio huko Gaza, inayolenga karibu watoto wachanga 600,000, imeanza Jumamosi hii ya tarehe 22 Februari 2025.
Katika takriban miaka mitatu tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, watu wa nchi hiyo wamevumilia mashambulizi ya mara kwa mara, “tishio la kisaikolojia, kufurushwa na mateso", ameonya Afisa wa uratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini humo Matthias Schmale leo Ijumaa, Februari 2025.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani WFP, limerejelea kwa kiasi usambazaji wa misaada ya chakula katika sehemu za Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), likitoa msaada muhimu wa lishe kwa wastani wa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miezi 59 waliokumbwa na utapiamlo, huku mapigano ya wiki tatu yakizidi kuathiri vibaya upatikanaji wa chakula kwa wale walio hatarini.
Mradi unaoendeshwa na serikali ya kenya na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru.
Wakati mapigano yalipozidi kushika kasi katika Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Francine Toyata alishikilia tumbo lake la ujauzito, maumivu yakimshika kwa wimbi la uchungu. Ilikuwa saa 2 asubuhi wakati alipoanza kusikia uchungu wa kujifungua, katikati ya eneo la vita. "Nimehamishwa mara mbili tangu Januari, na nilikuwa nikijificha katika kambi iliyojaa watu kupita kiasi," ameliambia shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu (UNFPA).
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya haraka inahoyitajika.
Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu.
Kutokomeza ukeketaji wanawake na watoto wa kike, FGM, ni jambo la dharura na linawezekana, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza kitendo hicho katili kinachokiuka haki za binadamu.