Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Ulaya

Mwanamke amesimama nje ya nyumba yake iliyoharibiwa na bomu huko Kharkiv, Ukraine.
© UNOCHA/Yurii Veres

Dunia isiipe kisogo Ukraine, dola bilioni 3.2 zahitajika kwa msaada wa  kibinadamu na wakimbizi: UN

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA na la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo yameisihi dunia kutoipa kisogo Ukraine huku yakisema dola bilioni 3.32 zinahitajika mwaka huu wa 2025 kwa asili ya kushughulikiamasuala ya kibinadamu na wakimbizi nchini humo.