Bangladesh: Ripoti yabainisha ushiriki wa viongozi wa juu katika ukandamizaji
Ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyofanyika nchini Bangladesh mwaka jana hadi kusababisha kuangushwa kwa serikali ya muda mrefu ya Waziri Sheikh Hasina ulisababisha vifo vya watu wapatao 1,400 ndani ya siku 46 pekee, wengi wao wakipigwa risasi na vikosi vya usalama, amesema hii leo Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu, Volker Türk, akinukuu ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR.