Vitisho lukuki vikikumba dunia, Guterres asema ushirikiano wa kimataifa ndio jawabu
Jumanne ya Februari 18, 2025 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi wa ngani ya mawaziri ukimulika umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kutekeleza kwa dhati makubaliano ya nchi wanachama juu ya uendeshaji wa dunia.