Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Wanawake

Mwanafunzi akipatiwa chanjo dhidi ya HPV katika kituo cha afya kusini magharibi mwa Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh

Fahamu mambo 5 kuhusu chanjo ya HPV na saratani ya shingo ya kizazi

  • HPV ni kifupi cha Human Papilloma Virus ambayo ni chanjo dhidi ya saratani  ya shingo ya kizazi.
  • Ina nafasi muhimu katika kutokomeza ugonjwa huu unaoathiri mamilioni ya wasichana na wanawake.
  • Katika kila dakika 2, mwanamke mmoja anakufa kutokana na saratani ya shingo ya kizazi.
  • Kuna baadhi ya maeneo idadi ya wagonjwa wapya ni ya juu hadi inatisha
Mkunga anayefanya kazi katika kliniki tembezi ya afya inayoungwa mkono na UNFPA akimkabidhi Francine binti yake mchanga, Amani.
© UNFPA DRC/Jonas Yunus

Nitamuita mtoto wangu Amani kwasababu amezaliwa katika vita, DRC

Wakati mapigano yalipozidi kushika kasi katika Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Francine Toyata alishikilia tumbo lake la ujauzito, maumivu yakimshika kwa wimbi la uchungu. Ilikuwa saa 2 asubuhi wakati alipoanza kusikia uchungu wa kujifungua, katikati ya eneo la vita. "Nimehamishwa mara mbili tangu Januari, na nilikuwa nikijificha katika kambi iliyojaa watu kupita kiasi," ameliambia shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu (UNFPA).

Mwanamke mmoja mjini Kigali, Rwanda, ameajiriwa katika kiwanda baada ya kusomea uhandisi.
© UN Women/Geno Ochieng

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN katika Siku ya Kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi

Miaka kumi iliyopita, maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yalitambua ukweli wa kimsingi; ushiriki wa wanawake ni muhimu kwa ajili ya kujenga ulimwengu bora kupitia sayansi na teknolojia. Nilijionea uwezo huo mkubwa nilipokuwa nikifundisha uhandisi, na niliona talanta ya ajabu, ubunifu, na azimio la wanasayansi wengi wa kike, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe  wake mahususi kwa ajili ya siku hii ambayo mwaka huu wa 2025 imetimiza muongo mmoja.

Fihya Al Tayeb Nasser mwenye umri wa miaka 13 ni mwanaharakati anayeoongza vuguvugu la haki za watoto kwenye jimbo la White Nile nchini Sudan.
UNICEF/UNI502078/Elfatih

Ushirikiano na harakati thabiti ni jawabu dhidi ya FGM: UNFPA, WHO, UNICEF

  • Je wajua! Leo hii wasichana na wanawake milioni 230 duniani kote ni manusura wa ukeketaji wanawake na wasichana, FGM?
  • Je wajua kuwa FGM ni ukiukaji wa haki za binadamu unaosababisha majeraha makubwa ya kimwili, kihisia na kisaikolojia kwa wasichana na wanawake.?
  • Je wajua bila hatua hivi sasa, ifikapo 2030 wanawake na wasichan milioni 27 watakuwa wanaishi wakivumilia ukiukwaji huu wa haki na utu wao ?
Rais wa Baraza Kuu Philémon Yang Yang akihutubia ufunguzi wa mjadala mkuu wa kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Laura Jarriel

Rais wa Baraza Kuu la UN awasilisha vipaumbele vyake kwa mwaka 2025

Philémon Yang Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo ameorodhesha maeneo makuu ya shughuli na matukio ya ngazi ya juu kwa mwaka huu wa 2025 akisema kuwa lugha mbalimbali na uwezeshaji wa wanawake itakuwa ni masuala mtambuka yatakayopewa uzito na kiongozi wa chombo hicho cha kujadili, changamoto zinazoikabili dunia ambazo zinahitaji kujitolea kufanya kazi pamoja.

Mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox’s Bazaar nchini Bangladesh.
ILO

Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha – Msichana Bangladesh

Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.

Sauti
1'40"