Mzunguko mpya wa chanjo ya Polio waanza Gaza
Mzunguko wa sasa wa kampeni kubwa ya chanjo ya polio huko Gaza, inayolenga karibu watoto wachanga 600,000, imeanza Jumamosi hii ya tarehe 22 Februari 2025.
Mzunguko wa sasa wa kampeni kubwa ya chanjo ya polio huko Gaza, inayolenga karibu watoto wachanga 600,000, imeanza Jumamosi hii ya tarehe 22 Februari 2025.
Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) iliyotolewa leo Februarai 20, 2025 inaonya kwamba uchumi wa Syria hautafikia kiwango chake cha kabla ya vita hadi mwaka 2080 kama ukuaji wa kiuchumi hautaongezeka kwa kasi.
Msaada wa kuokoa maisha leo umeendelea kufika Gaza huku wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakionya kuwa mahitaji bado ni makubwa baada ya miezi 15 ya mashambulizi ya anga ya Israel.
Umoja wa Mataifa leo umetaka msaada wa haraka wa kimataifa utolewe ili kukabiliana na janga la kibinadamu linaozidi kuwa baya nchini Syria, ambapo zaidi ya asilimia 70 ya watu wanahitaji msaada wa haraka.
Huku kukiwa na hofu kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano ya wiki tatu kati ya wapiganaji wa Hamas na Israeli yanakaribia kumalizika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza leo Jumanne, Februari 11 kuwa kurejea kwa vita huko Gaza lazima kuepukwe kwa gharama zozote.
Huko Mashariki ya Kati Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA Tom Fletcher alifanya ziara ya siku tatu huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya mateka wa Kiyahudi walioachiliwa na wafungwa wa Kipalestina waliotolewa gerezani kama sehemu ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza.
Karla Quintana, mkuu wa taasisi huru ya watu waliotoweka Syria IIMP, amehitimisha ziara yake ya kwanza mjini Damascus, akisisitiza umuhimu wa kushughulikia suala la makumi ya maelfu ya watu waliopotea.