Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Wahamiaji na Wakimbizi

Wanaume wawili wakishikilia makazi ya hema huku msimu wa hewa ya baridi ukiendelea huko Gaza.
UN News

Watoto watota kwa mvua Gaza, huku baridi kali ikitishia afya zao

Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya. 

Sauti
2'18"
Makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagala Kivu Kaskazini nchini DRC. (Maktaba)
© UNHCR/Guerchom Ndebo

DRC: Mashambulizi yakishamiri, sinfohamu yakumba wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya haraka inahoyitajika.

Sauti
2'37"
Raia wa Ethiopia wakiwasili Obock Djibout. Miongoni mwa  hao kuna vijana wanaoteswa wakifika Yeman
Olivia Headon/IOM

IOM na wadau watoa ombi la dola milioni 81 kuwasaidia mahamiaji Pembe ya Afrika, Yemen, na Afrika Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM) kwa kushirikiana na wadau 45 wa huduma za  kibinadamu na maendeleo,  leo mjini Nairobi Kenya, limezindua  ombi la dola milioni 81 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa wahamiaji zaidi ya milioni 1 na jamii zinazowahifadhi katika nchi za Djibouti, Ethiopia, Somalia, Tanzania, Kenya, na Yemen.

Mwanamume akibeba maji katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UN News

Muhtasari wa habari: DRC, Gaza na AI

Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.

Huko Kakuma nchini Kenya wakimbizi wafuga nyenje au Crickets ambazo ni chanzo cha protini.
WFP Video

Je, unafahamu kwamba nyenje ni chanzo cha protini?

Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Sauti
1'32"