Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Kimataifa

Bango la siku ya Lugha mama
UNESCO

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yatimiza robo karne

Maadhimisho haya yam waka huu ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yanaangazia robo karne ya juhudi za kujitolea kuhifadhi utofauti wa lugha na kuhimiza matumizi ya lugha za mama. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio, kurejesha ahadi, na kusisitiza jukumu muhimu la uhifadhi wa lugha katika kulinda urithi wa kitamaduni, kuboresha matokeo ya elimu, na kujenga jamii zenye amani na endelevu, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO).

Mwanafunzi akipatiwa chanjo dhidi ya HPV katika kituo cha afya kusini magharibi mwa Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh

Fahamu mambo 5 kuhusu chanjo ya HPV na saratani ya shingo ya kizazi

  • HPV ni kifupi cha Human Papilloma Virus ambayo ni chanjo dhidi ya saratani  ya shingo ya kizazi.
  • Ina nafasi muhimu katika kutokomeza ugonjwa huu unaoathiri mamilioni ya wasichana na wanawake.
  • Katika kila dakika 2, mwanamke mmoja anakufa kutokana na saratani ya shingo ya kizazi.
  • Kuna baadhi ya maeneo idadi ya wagonjwa wapya ni ya juu hadi inatisha
Watoto wakijifunza kwa kutumia kompyuta ndogo au tablet katika Shule ya Umma ya Melen ya Yaoundé, Kamerun.
© UNICEF/Frank Dejongh

Ukweli kuhusu dhana nne potofu kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni

Maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika makala hii iliyochapishwa kwenye wavuti wa shirika hilo leo Siku ya Kimataifa ya intaneti salama.

Mwanamke mmoja mjini Kigali, Rwanda, ameajiriwa katika kiwanda baada ya kusomea uhandisi.
© UN Women/Geno Ochieng

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN katika Siku ya Kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi

Miaka kumi iliyopita, maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yalitambua ukweli wa kimsingi; ushiriki wa wanawake ni muhimu kwa ajili ya kujenga ulimwengu bora kupitia sayansi na teknolojia. Nilijionea uwezo huo mkubwa nilipokuwa nikifundisha uhandisi, na niliona talanta ya ajabu, ubunifu, na azimio la wanasayansi wengi wa kike, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe  wake mahususi kwa ajili ya siku hii ambayo mwaka huu wa 2025 imetimiza muongo mmoja.

Mwanamume akibeba maji katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UN News

Muhtasari wa habari: DRC, Gaza na AI

Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.