Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mwanamume akibeba maji katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UN News

Muhtasari wa habari: DRC, Gaza na AI

Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.

Maiko Salali, mkazi wa Dodoma, Tanzania akizungumza kuhusu haki za watu wenye ualbino. (Maktaba).
UN/Tanzania

Tanzania: Mtaalamu wa UN apongeza uamuzi wa mahakama ya Afrika kuhusu watu wenye ualbino

Mtaalamu Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu wenye ualbino, Muluka-Anne Miti-Drummond, leo Februari 7 jijini Geneva, Uswisi amepongeza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, uamuzi ambao umeipata Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na hatia kwa kushindwa kuwalinda watu wenye ualbino dhidi ya mashambulizi ya kikatili, mateso, ubaguzi, usafirishaji haramu wa binadamu na utekaji nyara wa watoto wa watu wenye ualbino.

Ni katika mazingira ya kipee kabisa na yenye ushahidi usiopingika ndipo sheria za kimataifa zinaruhusu adhabu ya kifo (Kutoka Maktaba)
© UNICEF/Josh Estey

Ongezeko la kunyonga watu Iran linasikitisha sana - Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo  Januari 7 mjini Geneva, Uswisi amesema amesikitishwa sana na ongezeko kubwa la watu walionyongwa nchini Iran mwaka jana. Takriban watu 901 waliripotiwa kunyongwa mwaka 2024, arobaini kati yao wakiwa walinyongwa katika wiki moja pekee  mwezi Desemba. Takribani watu 853 walinyongwa mwaka 2023.