Wataalamu wa UN walaani vikwazo vya Marekani dhidi ya ICC
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu hii leo wameeleza wasiwasi wao mkubwa baada ya Rais wa Marekani kusaini Amri ya Kiuendaji inayoruhusu vikwazo dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wafanyakazi wake, na watu binafsi au washirika wake.