Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Bango la siku ya Lugha mama
UNESCO

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yatimiza robo karne

Maadhimisho haya yam waka huu ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yanaangazia robo karne ya juhudi za kujitolea kuhifadhi utofauti wa lugha na kuhimiza matumizi ya lugha za mama. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio, kurejesha ahadi, na kusisitiza jukumu muhimu la uhifadhi wa lugha katika kulinda urithi wa kitamaduni, kuboresha matokeo ya elimu, na kujenga jamii zenye amani na endelevu, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO).

Watoto wakijifunza kwa kutumia kompyuta ndogo au tablet katika Shule ya Umma ya Melen ya Yaoundé, Kamerun.
© UNICEF/Frank Dejongh

Ukweli kuhusu dhana nne potofu kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni

Maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika makala hii iliyochapishwa kwenye wavuti wa shirika hilo leo Siku ya Kimataifa ya intaneti salama.

Afrika ikigeuza changamoto kuwa fursa inaweza kuvuna dola trilioni 3.4
UNCTAD

Afrika ikigeuza changamoto kuwa fursa inaweza kuvuna dola trilioni 3.4- UNCTAD

  • Afrika inaweza kutumia biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kikanda ili kugeuza changamoto za kiuchumi kuwa fursa .
  • Afrika inaweza kuimarisha uchumi na kupunguza utegemezi wa masoko ya kimataifa yanayoyumba kwa kutumia Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), mageuzi ya kiuchumi, na  mbinu bunifu za kifedha.
  • Uwekezaji katika miundombinu, utofauti wa biashara, na biashara ndogo na za kati (SMEs) ndio msingi wa kufungua ukuaji na kusongesha maendeleo endelevu.
Mtaa moja jijini Dar es Salaam, bandari kubwa na ya kibiashara katika pwani ya Bahari ya Hindi nchini Tanzania. (Maktaba)
World Bank/Hendri Lombard

Juhudi za mahakama Tanzania kutekeleza SDG 16

Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linatilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.

Jorum Nkumbi, Mmoja wa walumbi wa lugha ya Kiswahili ambaye pia ni mwandishi wa vitabu nchini Tanzania akihudhuria kongamano la Kiswahili huko Havana, Cuba.
UN News/Kiswahili

Kukumbatia lugha nyingi ni nguzo ya ujumuishwaji katika jamii: Nkumbi

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linasisitiza kwamba kukumbatia uwepo wa lugha mbalimbali duniani ni muhimu kwa kukuza ujumuishwaji, utofauti wa kitamaduni, na maelewano miongoni mwa watu na pia kama njia ya kuhakikisha elimu bora, kuhifadhi lugha za asili, na kuhamasisha utangamno kati ya tamaduni hasa kujifunza kwa kutumia lugha ya mama.