Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Utamaduni na Elimu

Bango la siku ya Lugha mama
UNESCO

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yatimiza robo karne

Maadhimisho haya yam waka huu ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yanaangazia robo karne ya juhudi za kujitolea kuhifadhi utofauti wa lugha na kuhimiza matumizi ya lugha za mama. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio, kurejesha ahadi, na kusisitiza jukumu muhimu la uhifadhi wa lugha katika kulinda urithi wa kitamaduni, kuboresha matokeo ya elimu, na kujenga jamii zenye amani na endelevu, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO).

Mwanamke mmoja mjini Kigali, Rwanda, ameajiriwa katika kiwanda baada ya kusomea uhandisi.
© UN Women/Geno Ochieng

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN katika Siku ya Kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi

Miaka kumi iliyopita, maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yalitambua ukweli wa kimsingi; ushiriki wa wanawake ni muhimu kwa ajili ya kujenga ulimwengu bora kupitia sayansi na teknolojia. Nilijionea uwezo huo mkubwa nilipokuwa nikifundisha uhandisi, na niliona talanta ya ajabu, ubunifu, na azimio la wanasayansi wengi wa kike, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe  wake mahususi kwa ajili ya siku hii ambayo mwaka huu wa 2025 imetimiza muongo mmoja.

Dkt. Kisembo Ronex Tendo kutoka Uganda ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest.
UN News/John Kibego

Ni wakati wa kuachana na lugha za kikoloni na kukumbatia Kiswahili, Uganda tumeanza: Dkt. Kisembo

Wito wa shirika la umoja wa Mataifa la elimu  sayansi na utamaduni UNESCO wa kuinadi lugha ya Kiswahili miaka miwili iliyopita kama lugha ya kimataifa umepokelewa kwa mikono mwili na nchi mbalimbali barani Afrika na kutambua mchango wake ikiwemo Uganda itakayokuwa mwejeji wa kongamano la kimataifa la Kiswahili mwaka huu 2025 ikishirikiana na shirika la Afrika Mashariki Fest. Kwa nini Uganda imekivalia njuga Kiswahili sasa?

Mwanamume akibeba maji katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UN News

Muhtasari wa habari: DRC, Gaza na AI

Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.

Jorum Nkumbi, Mmoja wa walumbi wa lugha ya Kiswahili ambaye pia ni mwandishi wa vitabu nchini Tanzania akihudhuria kongamano la Kiswahili huko Havana, Cuba.
UN News/Kiswahili

Kukumbatia lugha nyingi ni nguzo ya ujumuishwaji katika jamii: Nkumbi

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linasisitiza kwamba kukumbatia uwepo wa lugha mbalimbali duniani ni muhimu kwa kukuza ujumuishwaji, utofauti wa kitamaduni, na maelewano miongoni mwa watu na pia kama njia ya kuhakikisha elimu bora, kuhifadhi lugha za asili, na kuhamasisha utangamno kati ya tamaduni hasa kujifunza kwa kutumia lugha ya mama.

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Bibirioni Limuru nchini Kenya wakionyesha mikanda ya mkononi inayotumika kulipia chakula .
UN News/Thelma Mwadzaya

Mlo shuleni isiwe kigezo cha kuchafua mazingira kuna nishati safi yafaa kupikia: UN/ Food4Education

Wakati dunia imeadhimisha siku ya nishati safi duniani mwishoni mwa wiki nchini Kenya hatua zinachukuliwa kwani bohari la shirika la Food4Education lililoko viwandani mjini Nairobi  ndio sehemu liliko jiko kubwa kunakoandaliwa kila siku chakula cha shule Kwa ajili ya wanafunzi wa kaunti ya Nairobi kwa kutumia nishati safi.