Mafunzo tuliyopewa na MONUSCO na biashara zetu vimeenda mrama baada ya M23 kutwaa Goma: Mnufaika
Goma, ambao ulikuwa mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC ulikuwa ni kitovu cha mafunzo ya ufundi stadi ya Umoja wa Mataifa kwa wanufaika wa miradi ya kusaidia jamii kiuchumi iliyolenga wapiganaji wa zamani waliokuwa wamejiunga na makundi yenye silaha, vijana walio katika hatari na wanawake walio katika mazingira magumu.