Ni wakati wa kuachana na lugha za kikoloni na kukumbatia Kiswahili, Uganda tumeanza: Dkt. Kisembo

Ni wakati wa kuachana na lugha za kikoloni na kukumbatia Kiswahili, Uganda tumeanza: Dkt. Kisembo
Wito wa shirika la umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO wa kuinadi lugha ya Kiswahili miaka miwili iliyopita kama lugha ya kimataifa umepokelewa kwa mikono mwili na nchi mbalimbali barani Afrika na kutambua mchango wake ikiwemo Uganda itakayokuwa mwejeji wa kongamano la kimataifa la Kiswahili mwaka huu 2025 ikishirikiana na shirika la Afrika Mashariki Fest. Kwa nini Uganda imekivalia njuga Kiswahili sasa?
Kupata jawabu mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye amezungumza na mwandaaji mwenza wa kongamano hilo Dkt. Kisembo Ronex Tendo, ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest
Licha ya changamoto ikiwemo mtazamo hasi kuhusu lugha ya Kiswahili nchini Uganda, kuna hatua za kujivunia ambazo zimepigwa, amesema Dkt. Kisembo Ronex Tendo.
Uganda ikiwa ni mwenyeji wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili litkaolofabyika tarehe 14 hadi 16 Aprili mwaka huu, Dkt. Kisembo amesema ni lazima mafanikio yaliopo yatumiwe kama msingi wa kupiga hatua Zaidi kukuza lugha ya Kiswahili kaika nchi zote za Afrika Mashariki.
Mtazamo wa Uganda kuhusu Kiswahili
Dkt. Kisembo ni Mkurugenzi wa shirika linaloweka vijana mstari wa mbele kuchagiza maendeleo ya Jumwiya ya Afrika Mashariki hasa matumizi ya lugha ya Kiswahil, liwalo Afrika Mashariki Fest lenye makao makuu jijini Kampala.
Amesema mtazamo wa hasi wa Waganda kuhusu lugha ya Kiswahili una mizizi yake katika vita vya Kagera mwaka 1979 ambapo wanajeshi wa Tanzania walimsaidia Dkt. Milon Obote kupidua serijali ya Idi Amini Dada wa Uganda.
“Chuki fulani ilijengeka hapo na Waganda wakaanza kuona Kiswaili kama lugha nzuri asema Dkt. Kisembo.
Amesema, Afrika Mashariki Fest kama mwaandalizi wa Kongamano la Kimataifa la lugha ya Kiswahili mwake huu, wanatoa kipaumbele kwa suala la kubadili mazamo kwa kueleza manufaa ya lugha kuliko historia.
Kuhusu hatua zilizopigwa na serikali ya Uganda chini ya utawala wa Raisi Yoweri Kaguta Museveni kukuza Kiswahili , Dkt. Kisembo amesema bunge la Uganda kupitisha Kiswahili kama lugha rasmi ni mafanikio makubwa.
Jingine muhimu sasa amesema ni kuanzisha mafunzo ya lugha ya Kiswahili katika shule zote za msingi, sekondari na tasisi za elimu ya juu.
Hata hivyo anasema, ni heri walimu wa Kiswahili waongezwe malipo ili kuwapa motisha kama ilivyofanywa kwa walimu wa masomo ya sayansi nchini Uganda.
“Sikubaliani na wanaosema walimu wa Kiswahili hawako Uganda kwa sasa. Wako lakini juhudi za kubadili mtazamo ni muhimu. Vituo vya redio vingekuwa vnatumia Kiswahili lakini hawajakitolea kipaumbele,” asema.

Ndani ya kongamano la kimaaifa la Kiswahili mwaka huu 2025.
Baada ya kongamano la mwaka jana mjini Havana nchini Cuba, Uganda wameamua kuambatanisha ziara za kitalii kama njia ya kupanua fursa za kijamii na kiuchumi.
Kwa maniki hiyo Dr. Kisembo amesema harakati muhimu zitaanza tarehe 13 kwa sherehe ya kumkumbuka hayati Mwalimu Julius Nyerere muasisi wa taifa la Tanzania ambako ni chimbuko la Kiswahili.
“Hiyo ni siku ya kuzaliwa kwake na kwa hiyo kama baba wa taifa tutakuwa na sherehe za kumkumbuka,” asema.
Kisha wataingia kongamano lenyewe tarehe 14 hadi 16 Aprili na kulitamatisha na ziara za kitalii kwenye sehemu mbai mbali muhumi ikiwemo mbuga ya wanyama pori ya Murchson Falls National Park na maporomoko ya maji.
“Kwani Uganda ni lulu ya Afrika, tulitambua umuhimu wa wageni wetu watembelee maeneo haya baada ya kuhuduria kongamano kama njia ya kukuza utalii wa ndani,” asema Dkt. Kisembo.
Maonesho ya bidhaa mbali mbali vikiwemo vitabu vya lugha ya Kiswahili yatakwenda sanjari na kongamano hilo.
Hongera kwa Raisi Museveni na BAKITA
Dkt. Kisembo amesema aliomba komgamano la mwaka huu lifanyike Uganda alipo hudhuria kongamano la mwaka jana nchini Cuba.
“Nilialikwa na Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania BAKITA kuwakilisha Uganda na nilipomwambia Raisi Museveni kuhusu mwaliko huo alikubali nikawakilishe Uganda na kufadhili safari hiyo asilimia 100” amesema.
Namshukuru sana pamoja na serikali ya Tanzania,” ameongeza Dkt. Kisembo akiongea na John Kibego wa UN News jijini Kampala.

Kuhusu umihimu wa lugha ya Kiswahili:
Dkt. Kisembo amemalizia kwa kusema “Hauwezi kudai uhuru wakati ambapo hautumii lugha yetu inayouunganisha kama Wafrika”
Kwani amesisitiza kuwa “Kiswahili ni lugha unganishi kijamii na wezeshi kibiashara kwa hiyo ni kwa bahati mbaya kuona kwamba hata kwenye vikao vya serikali zetu Kifaransa na Kingereza ndivyo vinatumiwa badala ya Kiswahili”