Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene
Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo.
Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia.
Mmoja wa wakishiriki hao kutoka Kenya na Mary Wambui Munene akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili amesema kazi anayoifanya Kenya ya lama mwenyekiti wa taasisi inayoshughulika na familia za mitaani ambazo zinajumuisha watoto, kina mama na vijana ndio iliyomuwezesha kuja kwenye mkutano huu.
Juhudi za serikali ya Kenya kusaidia familia za Mmitaani
Kwa mujibu wa Mary Wambui serikali ya Kenya ilianza kutoa kipaumbele katika suala la familia z mitaani mwaka 2003 lengo likiwa kuwasaidia watoto wa mitaani, wanawake walioolewa na vijana wa mitaani ambao wamekulia mitaani na waanza familia zao mitaani.
“Tunachokifanya ni kufika mitaani kuchukua watoto na vijana hao , kisha tunawepeleka katika vituo maalum wanapatia msaada wa tina na ushauri nasaha , dawa , mahali pa kulala na chakula “
Ameendelea kusema kua baada ya muda sasa wananza kufundishwa jinsi ambavyo wataweza kujitegemea kwa kupewa mafunzo ya ujasiriamali kama kushona nguo, ususi wa nywele na kutengeneza bidhaa za shanga vitu ambavyo vinawaingizia kipato cha kuweza kujitegemea

Kuhusu mkutano wa ECOSOS wa maendeleo ya jamii
Bi. Wambui Munene amesema mkutano huu muhimu unahusu maendeleo ya ustawi wa jamii ambapo wadau kutoka nchi mbalimbali wanajadili jinsi ya kuziinua jamii lhasa makundi ya watu mbalimbali wasiojiweza ikiwemo wazee, watoto na wanawake na vijana.
Mathalani amesema “Sisi Kenya tumeshaanza mipango ya kuinua jamii zetu mfano wazee kuanzia umri wa miaka 70 yunawapatia pesa ili wawze kujikimu ili wasitaabike sana wakati ambapo wenzi wao wameaga dunia, au watoto wao wameshaondika katika boma na mama anajikuta hana mtu wa kumsaidia. “
Hivyo amesema serikali ya Kenya iliona ni muhimu kuwasaidia watu wa kundi hii kupitia mradi wa inua jamii.
Masuala muhimu waliyojadili katika mkutano huo ni kuhakikisha dunia inakuja pamoja ili kuzinusuru jamii zao. Jinsi gani wanaweza kuwasaidia na kuhakikisha watoto wanapata fursa ya elimu.
Matarajio yake katika mkutano huu
Wambui anasema katika mkutano huu ana matarajio makubwa ikiwemo “kuchukua kile tulichojadili kuhusu kuinua jamii na hasa jinsi ambavyo tunaweza kusaidia vijana wote wavulana na wasichana waweze kupata ajira.
Alipoulizwa endapo mpago huu wa inua jamii ni wa kila mtu Kenya na watu wanaufahamu? Bi. Wambui Munene amesema “kile ambacho tunafanya ni kwamba tulianza Kwenda mitaani kuwasaka hususan wale watu wasio na makazi wanaolala kwenye mitaro, hawana chakula na hawana mtu wa kuwasidia , tunazungumza nao na kuwajulisha kwamba tunataka kuwasaidia.”
Ingawa si kazi rahisi anasema wanawashawishi kutoka mtaani ili waweze kupatiwa mahali ambako wataweza kula, kuoga na kufanya mambo mengine, na wakakubali.
Baada ya mafunzo nini kinafuata
Mwenyekiti huyo amesema cha kwanza “Tunawasaidia kidogo kwa kuwalipia nyumba miezi sita , na mahali wanapofanyia kazitunawapatia vitendeakazi”.
Ameendelea kusema kuwa na baada ya muda wanakuwa na uzowefu na kisha wanaanza kujitegemea.
Bi. Wambui anasema dhamira ya mradi wa inua jamii ni kuhakikisha wameweza kuzitoa familia nyingi kadri iwezekenavyo mitaani na kuzisaidia.