Mafunzo tuliyopewa na MONUSCO na biashara zetu vimeenda mrama baada ya M23 kutwaa Goma: Mnufaika
Goma, ambao ulikuwa mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC ulikuwa ni kitovu cha mafunzo ya ufundi stadi ya Umoja wa Mataifa kwa wanufaika wa miradi ya kusaidia jamii kiuchumi iliyolenga wapiganaji wa zamani waliokuwa wamejiunga na makundi yenye silaha, vijana walio katika hatari na wanawake walio katika mazingira magumu.
Lakini baada ya kutwaliwa kwa mji wa Goma na wapiganaji wa kundi la M23, miradi hiyo iliyotekelezwa na kitengo cha kuvunja makundi, kusalimisha silahaa na kujumuishwa kwenye jamii, DDR cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini DRC, MONUSCO, imesambaratika.
Miongoni mwa wanufaika jimboni Kivu Kaskazini akizungumza na UN News amejitambulisha akisema anaitwa Valérie Mubawa, ni mwanafunzi nimejifunza kuendesha pikipiki na kuzitengeneza. Tulifunzwa na Umoja Wa Mataifa kupitia kikundi cha MONUSCO".

Baada ya mji wa Goma kuvamiwa na kutwaliwa na kundi la wapiganaji Mama Valérie anasema tulipomaliza mafunzo baada ya wiki moja vita ikaingia mjini watu walikimbia huku na kule wengine walibaki lakini sisi ambao tulibarikiwa kubaki mjini tuliweza kuchunga vitu tulivokua navyo.”
Anasema walikuwa wameanza kazi yao lakini wiki mbili hakukuwa na kazi sababu watu walikuwa katika wasiwasi wengine walikimbilia mbali hata yule mteja ambaye ungebeba hana pesa na ilikuwa ni kuogopa uporaji uliokuwepo na ilitusukuma kukinga vitu kuweka nyumbani sababu vitu vyetu ni vipya na kulikua wezi wa pikipiki".
Maisha ya wajarisiamali wa bodaboda yamepinduliwa ambapo anasema “wakati huu kuweza ni vigumu sababu watu tunaowabeba na kuwatumikia hawana pesa na benki zimefungwa hakuna pa kupata pesa na wale wa kutupatia kazi hawana uwezo wa kulipa.”
Hatuwezi kulipa marejesho, tuna hofu hata ya kupakia abiria
Ameongeza kuwa kuna changamoto lukuki anazopitia wakati huu vita ikiendelea Mashariki mwa DRC . “Inafaa kufanya kazi huku tukipeleka fedha kwenye vikundi vyetu ya ushirika. Sasa wakati vita vimeanza mtu hakuweza kufikisha kiasi cha pesa hiyo kama ni pikipiki wanaomba ulete dola 25 kila wiki, bajati dola 75 sasa haikuwezekana sababu ya vita, sababu watu hawana pesa, watu wanaogopa kuingia barabarani sababu unawaza pia utapokoingia barabarani utakutana majambazi na watakupora pikipiki. Tunafanya kazi na wasiwasi kila mtu anayekusimamisha unamuogopa unapomuona unawaza akatupora chombo chako".
Wito wake kwa jumuiya ya kimataifa
Mama Valérie ana wito kwa jumuiya ya kimataifa akisema" Ombi letu ni kwamba amani kwanza sababu amani ikiwepo kila kitu kitawezekana kwani hatuwezi kuogopa mwenzako utamuona pasipo na woga ukipendelea kwenda kufayakazi uende Kibumba, Kibati, Mugunga, uende Saké uende popote kwenye utapata fedha bila kuogopa lolote. Sasa watusaidie amani idumu ".
Na kisha akaugeukia Umoja wa Mataifa akisema "oOmbi letu ni kwamba Umoja wa Mataifa utazame kwamba wametufundisha kazi na inabidi hiyo kazi tufaidike nayo kwa sababu wametufunza kazi ili tubalishe maisha tusirudi katika maisha yetu ya kale, ili tuingie katika maisha ya raha na kufuraia kazi tuliopewa na tuone watoto wanasoma tupate pesa kulipa shule.”
Kusoma zaidi kuhusu mradi wa mafunzo waliyopata Mama Valérie bofya hapa.