Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanahabari wakumbatia kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini DRC

Rose Mabbulo, mwanahabari wa Terra FM akiwa na waandishi wa habari wenzake kwenye harakati za kuhamasisha jamii kuhusu usimamizi wa taka za plastiki na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla huko Ramogi, Mukambo DRC.
UN News/John Kibego
Rose Mabbulo, mwanahabari wa Terra FM akiwa na waandishi wa habari wenzake kwenye harakati za kuhamasisha jamii kuhusu usimamizi wa taka za plastiki na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla huko Ramogi, Mukambo DRC.

Wanahabari wakumbatia kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini DRC

Tabianchi na mazingira

Katika mji wa Ramogi, Mukambo jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wanahabari wanaonekana wakiongoza juhudi za kuodoa taka ya plastiki na taka zingine kutoka mifereji ya sokoni.

Rose Mbulabo, mwanahabari wa kike kwenye Terra FM -  redio iliongoza harakati za maadhimisho ya siku ya redio duniani katika eneo la Mahagi, anaonekana kwenye lori akiongea kwa sauti kuu akichagiza wakaazi kushiriki juhudi za kuepusha mazingira, taka ya plastiki.

Mifuko hii ya plastiki inaweza kudumu kwa miaka mingi bila kuoza, anasema kwa sauti kuu Bi. Mbulabo.

“Watoto na wajukuu wetu watakuwa namna gani ikiwa hatujali kulinda mazingira? Ni jukumu letu kuhakikisha usalama wa mazingira leo,” aongezea Bi. Mbulabo.

Jamii za eneo la Mhagi nchini DRC wakishiriki ziku ya kukusanya taka za plastiki na kusafisha mazingira kufuatia hamasa kutoka kwa wanahabari.
UN News/John Kibego
Jamii za eneo la Mhagi nchini DRC wakishiriki ziku ya kukusanya taka za plastiki na kusafisha mazingira kufuatia hamasa kutoka kwa wanahabari.

Wanahabari kutoka redio zaidi ya 13 zilizomo katika eneo la Mahagi wameshirikiana kuweka katika mafanikio wajibu wao wa kuhabarisha na kuhamasisha jamii tofauti na maangazo ya redio.

Samwel Mungu Rom Atido, mtangazaji kwenye Redio FDC iliyoko mjini Mahagi ameipongeza Terra FM na shirika la Environmental Defenders (ED) kwa kuwalea pamoja wanahabari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya redio duniani.

“Imekuwa fursa ya kuhamasisha wasikilizaji wetu uso kwa uso tukishirikiana na wadau wengine kama wale wa mashirika ya kiraia na viongozi wa serikali,” anasema Mungu Rom Atido.

Sarah Lonyo kutoka Terra FM anasema harakati hizi zitatumia kama msingi wa kwimarisha juhudi za uhamasishaji i kuhusu mabadiliko ya tabianhci katika ushirikiano chini ya mwavuli wa wanahabari sio kama vituo vinavyowajiri.

“Tumekusanya taka na kuzichoma moto tukishirikiana na jamii kama ishara kwamba tunatia katika mafanikio kile tunachosema kupitia matangazo ya redio,” asema Lonyo.

Redio imepanda miti

Harakati hizi zilianzia sehemu ya mpakani na Uganda ya Kolokoto

Kwa upande wke Mohamad Urom Musa, redio imeleta nuru katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Kuna ahueni sasa kwani unaona watu wakipanda miti na hali ya joto ikiwa haipandi juu zaidi kama ilivyokuwa kabla ya redio kuimarisha uhamasishaji. Terra FM na redio zingine wamefanya kazi kubwa,” anasema Urom.

Modest Ugenrwoth Unen, Mwakilishi wa Chifu wa Mukambo kwenye mmoja wa mikutano ya uhamasishaji mjini Ramogi, anawatolea wito watu wote kuchukua ujumbe wa kulinda mazingira hadi majumbani.

Waandishi wa habari wa wilaya ya Mhagi wakijadiliana kuhusu mazingira ya kazi katika siku ya mazingira duniani katika kanisa la Ramogi, Mukambo DRC.
UN News/John Kibego
Waandishi wa habari wa wilaya ya Mhagi wakijadiliana kuhusu mazingira ya kazi katika siku ya mazingira duniani katika kanisa la Ramogi, Mukambo DRC.

“Tusiuache ujumbe huu hapa bali tuupeleke majumbani,” asnasisitiza.

Robert Agennga, mwanaharakati wa mazingira na haki za binadamu, katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda na DRC amesema redio wanakumbuka siku ya redio dunaini kwa sababu redio imesalia chombo muhumu cha kuhamasisha jamii barani Afrika.

“umeona redio ikipanda miti, redio ikilinda mazingira na unaamini itaendelea kusaidia kwa miaka zaidi ya  200 barani Africa,” asema Bwana Agenonga.

Kwa mujibu wake, kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba hali ya joto haipandi Zaidi ya nyuzi joto 1.5 za selusiasi pasipo na uhai.

Akiwa ni mmoja wa washauri wa bodi ya usimamizi wa shirika la Environmental Defenders amesema, walitumia fursa hii ya wanahabari kukutana na kuwapatia mafunzo kuhusu usalama wao wanapofanya kazi.

“Pia tumewakumbuka wanahabari waliopoteza maisha yao wakifanya kazi ya kuchunguza masuala nyeti kuhusu biashara haramu ya mbao kwa mfano,” asema.

Benjamin Jeremie, kiongozi wa vijana wa Mukambo amesema atasogeza ujumbe kwa vijana wote ili wahiriki kikamilifu kaika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mashindano ya mbio miongoni mwa watu wenye uzio wa Zaidi ya kilo 70 ni sehemu ya harakati zingine zilizotumiwa kuvutia wakaazi  wa sehemu za Kolokoto na Ramogi ili wapokee ujumbe kuhusu mazingira.

Washindi walipewa zawadi za hadi karibu dola 20 za kimarekani kwa kuzunguka mara mbili  uwanja wa mpira wa miguu.